Saturday, September 15, 2012
WATOTO WENYE VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA KUVALISHWA UTEPE MWEKUNDU
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kibaha mkoa wa pwani amesema kuwa amepokea maombi ya wazazi ambao watoto wao wameathirika na vvu kuwa watoto hao wavae utepe mwekundu ili wasifanye kazi ambazo zitachangia kudhoofisha afya zao.
Tanzania ina idadi takribani ya watu milioni 1.4 walioambukizwa vvu,idadi ambayo ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki,Na katika idadi hiyo wanawake ndio wanao ongoza kwa maambukizi yakitoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Lakini sheria ya Tanzania hairuhusu mtu kumatangaza mtu yeyote kuwa ameathirika na adhabu yake ni miaka mitatu jela.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment