Friday, September 28, 2012

HIZI NDO NYIMBO TANO AMBAZO RICK ROSS ATAZISHUSHA NDANI YA FIESTA DAR ES SALAAM.



Ukweli umejulikana jana kuwa Rick Rozay ndiye msanii atakayatua kwenye Fiesta ya Dar es Salaam itakayofanyika October 6, 2012. 

Hapa Clouds FM wamepiga bao. Bosi huyu wa Maybach Music Group anakubalika kinoma noma na wapenzi wa Hip Hop wa Bongo.

Ana bahati kuwa anapendwa na kila aina ya wapenzi wa hip hop kuanzia wasichana, wagumu, mabrazamen na hata watu wazima kiasi. Hii ni show itakayoacha gumzo hata kama akitumbuiza kwa kiwango cha kawaida tu. 

Angalizo: Watu wasitegemee dancers kama wa Diamond kukata kiuno wakati the boss himself atakapokuwa stejini!! ‘Hip hop sio mauno ni Dj’ alisema Ngweir kwenye 120, unakumbuka?

Rick Ross ana ngoma kibao ambazo tuna uhakika uwanja mzima wa Leaders, Kinondoni utakuwa ukimuitikia mwanzo mwisho! So tumeziangalia nyimbo tano ambazo tuna uhakika ndizo zitakazowasha moto pindi atakapozitumbuiza, nazo ni:

1. The Boss Ft. T.Pain
Ngoma hii ipo kwenye albam yake ya mwaka 2008, Trilla. Beat imenyongwa na producer mzaliwa wa Afrika Kusini, J.R Rotem. Chorus imefanywa na T-Pain.

2. Hustlin
Hii ndio ngoma iliyomtambulisha vizuri Rick Ross kimataifa. Ni ngoma iliyopo kwenye albam yake ya kwanza iliyotoka mwaka 2006, Port of Miami. Ina bonge la beat ambalo lilitengenezwa na The Runners.

 Hii ndio ngoma iliyotengeneza idendity yake kama rapper mnene, mwenye ndevu nyingi lakini mwenye uwezo wa aina yake katika kuchana. Mashabiki wake wa Dar wakiisikia ngoma hii atawakumbusha mbali sana hasa chorus yake yenye sauti zilizo shushwa pitch ‘Every day I’m hustlin every day I’m hustling…………”


3. Aston Martin Music

Kama ingetokea angekuja na Drake kwenye show yake ya Dar, pangekuwa hapatoshi kwenye eneo la tukio. 

Ngoma hii iliyotengenezwa na kundi la maproducer walio karibu sana na Rick Ross la J.U.S.T.I.CE League, ina bonge moja la beat na chorus tamu isiyo na mfano kutoka kwa Drizzy Drake na mrembo Chrissete Michelle. Tuna uhakika wabongo watakuwa wakiimba chorus hii bila shida.

4. Blow Money Fast (BMF)
“I think I’m Big Meech, Larry Hoover Whippin’ work, hallelujah One nation under God Real niggas getting money from the f***ing start” rudia tena!! There no way umati wa mashabiki utakaohudhuria kwenye Fiesta unyamaze na kuacha kufuatiliza chorus hii. Na beat lake je? Lex Luger hakufanya mchezo kabisa hapa. Kwa ngoma hii, ujio wa Rick Ross utakamilisha utamu wake na roho za watu zitakongwa vilivyo. 

5. Imma Boss
Well, hii si ngoma ya Rick Ross bali ni ya kijana wake wa MMG, Meek Mill. Ngoma hii ina beat moja matata mno na jinsi ilivyo maarufu Tanzania, Rick Ross hana ujanja wa kukwepa kuiperform!!! 


No comments:

Post a Comment