Tuesday, July 24, 2012

WANAVIJIJI 37 WAKRISTO WAUWAWA NIGERIA

Mashambulio kadha yameshawahi kufanywa Nigeria

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Mustapha Salisu, alisema askari wa usalama walipigana vikali kwa saa kadha, na wale aliosema walikuwa washambuliaji wajuzi.
Alisema zaidi ya washambuliaji 20 waliuwawa.
Msemaji wa kikundi cha Wakristo alisema vijiji 13 vilishambuliwa.



SHAMBULIO LA BOMU LAUA MTOTO WA SHULE HUKO NIGERIA

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka kumi amefariki baada ya kombola kutua katika shule hiyo mjini Jos, Nigeria.
Kwa mujibu wa maafisa wakuu, kombora hilo lilikosa lengo lake na badala yake kugonga jengo moja karibu na shule hiyo.
Maafisa wa shule wanasema kuwa mtoto huyo hakuwa mwanafunzi katika shule hiyo kubwa inayomilikiwa na jamii ya kiisilamu.
Mwandishi wa BBC mjini Jos, Ishaq Khalid anasema kuwa wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wanafanya mitihani yao wakati wa shambulizi hilo.
Mji wa Jos uimekuwa kitovu cha mapigano ya kikabila pamoja na mapigano ya kidini katika miaka ya hivi karubini.,
Jos ni mji mkuu wa jimbo la Plateau ambalo liko katika eneo linalogawanya maeneo ya kikristo na yale ya kiisilamu ya Kaskazini.

Habari na BBC.

MWANDISHI WA ETHIOPIA AFUNGWA JELA MIAKA 18

   

NI KUTOKANA NA KUKIUAKA  SHERIA YA UGAIDI.


Eskinder Nega na wenzake 23 walipatikana na hatia mwezi uliopita.
Walikamatwa kwa madai ya kuwa na uhusiano na kundi moja la upinzani lililo na makao yake Marekani kwa jina Ginbot Seven.
Serikali ya Ethiopia inadai kuwa kundi hilo ni la kigaidi.
Mahakama hiyo ya Addis Ababa pia ilimfunga jela maisha mwanaharakati wa upinzani,Andualem Arage.
Kutokana na kazi yake ya uwana-habari na kuandika Blogi, Mwezi wa May, Eskinder alipewa tuzo maarufu la kimarekani la Pen America's Freedom to Write.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu zimekuwa ikiilaumu serikali kwa kubuni sheria hiyo ya kukabiliana na ugaidi yakisema sheria hiyo haifai.
Siku ya Ijumaa Mwanahabari ,Eskinder na mwanachama wa chama cha upinzani cha Unity for Democracy and Justice party walikuwa mahakamani kuhukumiwa.
Washukiwa wengine 16 waliopatikana na hatia mwezi wa Juni wako ukimbizini.
Walipokuwa wakiingia mahakamani wawili hao waliwapungia mikono jamaa zao na marafiki pamoja na maafisa wa kibalozi waliokuwemo ndani.
Eskinder alikamatwa mwezi wa Septemba mwaka jana baada ya kuandika makala iliyokuwa ikiilaumu serikali ya Ethiopia kwa kukamata wapinzani wake kwa kutumia sheria ya ugaidi.
Miongoni mwa watu ambao wamekamatwa chini ya sheria hiyo ni msanii na mcheza filamu maarufu nchini Ethiopia, Debebe Eshetu ambaye ni mkosoaji mkuu wa serikali.


Monday, July 9, 2012

WAKAMATWA WAKIMSAFIRISHA MTOTO MCHANGA KIMAGENDO AKIWA KATIKA BEGI

Sharjah Airport - baby Smuggers

Mume na mke wenye asili ya Kiarabu walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Sharjah mara tu walipotua katika ardhi ya United Arab Emirates.
Mtoto huyo aligundulika na miale ya X-ray, wazazi wa mtoto huyo walisema kuwa iliwabidi kufanya hivyo sababu mtoto huyo hakuwa na nyaraka zozote za kusafiria na walikuwa wanataka kuwa nae katika hiyo safari yao.
Wazazi wa mtoto huyo wamefunguliwa mashtaka ya kuhatarisha maisha ya mtoto wao baada ya kumsafirisha katika begi na kupigwa na miale mikali ya x-ray.

 X-ray ... the baby was spotted in luggage

picha ya x-ray ikimuonesha mtoto ndani ya begi.

MTOTO MWENYE VICHWA VIWILI AZALIWA BRAZIL

Mother's pride: The mother insisted she was delighted with her newborn who weighed 9.9lbs  


Katika mji wa Anajas huko nchini Brazil katika hospitali ya Santa Casa, mtoto ambae ana vichwa viwili amezaliwa akiwa na afya njema, Daktari mkuu wa hospitali hiyo amesema kuwa mama wa mtoto huyo ambae ana umri wa miaka 25 alitakiwa kuzaa mapacha ila kwa bahati mbaya hakufanyiwa vipimo vya ultra sound mapema .
Ubongo wa vichwa vyote unafanya kazi vizuri ingawa anatumia moyo mmoja, mpafu,ini pamoja na uti wa mgongo.
Pia dokta alisema kuwa hawafikirii kufanya upasuaji kwa sasa kwakua ubongo wa vichwa vyote viwili unafanya kzai sawa..."changamoto tuliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha tunatunza vyema afya ya mtoto huyu" alisema Daktari mkuu wa hospitali hiyo ya Santa Case.