A-Z ya watu mashuhuri duniani

RIHANNA

Rihanna 

Jina kamili: Robyn Rihanna Fenty
kazi yake:  Mwanamziki
Umri: 24
Alipozaliwa: St.Michael Parish,Caribbean island of Barbados
Tarehe ya kuzaliwa: 20 feb 1988

Rihanna ni mtoto wa familia ya watoto watatu, mama yake (Monica Fenty) ambaye ni muhasibu na baba yake ni (Ronald Fenty) ambae alikuwa msimamizi mkuu wa godown.

Rihanna  
Alipofikisha umri wa miaka 14 wazazi wake walitengana kwa kupeana taraka.
Maisha ya Rihanna hayakuwa maraisi sababu baba yake hakuwa akimjari sana kwani mara nyingi Rihanna alipokuwa akifanya makosa baba yake alikuwa akimungalia tuu.
Kwakuwa baba yake alikuwa ni mlevi  kupindukia wa pombe ilimlazimu Rihanna kuhangaika yeye mwenyewe kujiokoa katika maisha magumu.

Alipofikisha umri wa miaka 15 alitengeneza kundi la wasichana tupu pamoja na rafiki zake wawili aliokuwa akisoma nao.
Alikutana na producer mkongwe (Evan Rogers) ambae alikwenda kuishi nae nyumbani kwa producer huyo.
"nilipoondoka Barbados sikuangalia nyuma", "nilitakiwa kufanya nilichotakiwa kufanya hatakama itanibidi kwenda Marekani" alisema Rihanna alipokuwa akitengeneza demo ya wimbo wake wa nne.

Rihanna 

Katika umri wa miaka 16 Rogers alimpeleka Rihanna katika studio ya Def Jam iliyokuwa chini ya Jay-z kwa ajiri ya majaribio ya kupata mkataba.
Jay-Z alimsikiliza Rihanna kwa Makini na kujutia kwa nini Rogers hakumpeleka mapema mwana dada huyo.
Jay-Z alimsainisha mkataba Rihanna papo hapo.
  

Mwaka 2005 mwezi wa 8 Rihanna alittoa nyimbo kali ilijulikana kama "Pon de replay" iliyoshika nafasi ya pili katika Billboard, mwezi uliofuata alitoa album yake aliyoipa jina la "music of the sun" mwaka uliofuata alitoa album ya pili iliyoitwa "A girl like me" iliyobeba nyimbo kali kama vile "unfaithfull na SOS".

Katika mwaka wa 2007 Rihanna  alibadilika kutoka teen cute pop hadi full super star na album yake ya tatu ya "Good girl Gone Bad" iliyobeba nyimbo ya "umbrella" aliyomshirikisha Jay-Z iliyompatia tuzo ya grammy.

HIYO NDO HISTORIA FUPI YA RIHANNA TANGU ALIPOTOKA MPAKA SASA NI MWANAMUZIKI MKUBWA DUNIANI.
(people.com,bio.true story).














GADDAF

Muammar Gaddafi alizaliwa jangwani karibu na Sirte mwaka 1942.
Gaddafi katika mkutano Sirte
Gaddafi katika mkutano Sirte
Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri na, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.
Gaddafi alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya, mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa 1969.
Ghaddafi alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Gaddafi alipokuwa akizuru Senegal mwaka 1985
Gaddafi alipokuwa akizuru Senegal mwaka 1985
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Hema ya Gaddafi
Hema ya Gaddafi
Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, huwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema hiyo pia hutumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.

Benjamin Barber, mtaalam wa kisiasa wa kujitegemea, kutoka Marekani amewahi kukutana na Gaddafi mara kadhaa hivi karibuni na kuzungumza naye kuhusu mustakabali wa Libya.
Gaddafi akiwa na viongozi wengine wa nchi za Uarabuni
Gaddafi akiwa na viongozi wengine wa nchi za Uarabuni
Bw Barber alisema kuwa Muammar Gaddafi anajihisi kuwa msomi aliyebobea.
Muammar Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 29 Mei 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.
"Utashangazwa kuwa ingawaje ni dikteta, ni mwanafalasafa na mwenye kutafakari jambo kabla ya kuzungumza," aliiambia BBC.
"Namchukulia sana kama mtu kutoka kabila la Waberber na mtu ambaye aliibuka kutoka tamaduni za watu wa jangwani, kutoka kwenye mchanga na kwa namna fulani kuna tofauti kubwa na uongozi wa kisasa, na kwa namna fulani hilo limemfanay awe mstahamilivu na mwenye msimamo."
Kanali Gaddafi amejitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou, kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.
Hivi karibuni aliongoza jitihada za kuwapatanisha waasi wa Tuareg kutoka nchi za Niger na Mali.

'Mbwa kichaa'

Jumuiya ya wanadiplomasia kuitenga Libya kulitokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation Organisation.
Gaddafi akiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Gaddafi akiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.
Ilisemekana kuwa Kanali Gaddafi alitikiswa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.
Muuguzi wa Gaddafi
Muuguzi wa Gaddafi
Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano kati ya Washington na Libya.
'Hakutakuwa na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi' Kanali Gaddafi alisema alipokuwa akiiherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.
 (BBC swahili).







cristiano ronaldo 

 

 

Jina kamili: Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro
Tarehe ya kuzaliwa:February 5, 1985,
Alipozaliwa:Madeira, Portugal
Cristiano an kaka mmoja aitwae Hugo, na dad wawili Elma na Liliana.
kutokana na kumpenda sana Rais wa zamani wa Ureno aliekuwa akiitwa Ronaldo Reagan, baba yake aliamua kumpa jiana hilo.
katika kisiwa cha Mederia ndipo Ronaldo alipojifunzia soka, na alipofikisha umri wa miaka 12 alikuwa tishio katiaka soka katika kisiwa hicho. Mpaka hapo Ronaldo alikuwa tayari amejipatia ujiko katika timu kubwa kama vile Porto,Buevista n.k, ingawa baada ya hapo aliamua kuelekea katika timu ya Sporting lisbon.
kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier aliona kipaji chake wakati huo Ronaldo akiwa na miaka 16 lakini hakumsainisha mkataba kwakuwa alimuona bado mdogo na alikuwa akihitaji mafunzo zaidi.
Katika mwaka wa 2003 kipindi cha majira ya joto Man U ilicheza na Sporting na Man U ilichezea kichapo, hapo ndipo Jicho la Sir Alex Furguson liliponasa kwa Kinda huyo, na Ronaldo ndie alikuwa mchezaji pekee wa Kireno kuchezea Manchester United.
Kwa mara ya kwanza alichagua jezi namba 28 kwakuwa alijua hataweza kuimudu presha ya jezi namba 7 iliyovaliwa na wachezaji waliokuwa hatari katika timu hiyo kama vile George Best, Eric Cantona, na David Beckham.
Katika mwaka wa 2006 alipata upinzani mkubwa kwa washabiki wa England baada ya kumchomea mchezaji mwenzie (Wyne Rooney) kupewa kadi nyekundu katika robo fainali ya kombe la dunia Ureno ilipokutana na Wingereza, lakini hakukata tamaa naalirudisha tena matumaini na upendo kwa mashabiki hao baada yamwaka 2007 kushinda tuzo zifuatazo:  "mchezaji chipukizi wa mwaka" "mchezaji bora anependwa na mashabiki wa mwaka" "mchezaji bora wa ureno wa mwaka"
Anapenda: kupika
huwa anapika kbla ya kwend mzoezini
Hapendi: kuvuta sigara,watu ambao siyo wakarimu, na watu wasipenda kujituma.
                            

 




OPRAH WINFREY


 

Moja ya vipindi vinavyotazamwa sana katika historia ya Marekani, The Oprah Winfrey Show, kinamalizika baada ya miaka 25. Kipindi chake kimegusa wengi na kuvuka mipaka ya televisheni.
Kipindi chake cha kwanza, kilichoitwa Namna ya Kumwoa au Kuolewa na mtu wa Chaguo lako, kilipendekezwa kiwe kipindi kinachorushwa mchana kama kipindi chengine chochote cha kawaida.
Lakini baada ya vipindi 4,560, watu maarufu kama Madonna, Beyonce na Tom Hanks wanatarajiwa kutokea kwenye kipindi chake cha mwisho cha kuagwa, kinachorushwa hewani siku ya Jumatano.
Wakati wa miaka hiyo 25, Winfrey limekuwa jina maarufu sana, anayekubalika na wengi na ni mmoja wa matajiri katika ulimwengu huu.
Akimaliza na kuendelea kufanya kazi katika televisheni yake mwenyewe, uwezo wa kupata wageni wanaovutia kwenye habari haliwezi kudharauliwa.
Mwezi huu, Rais Obama alizungumzia kwanini alihitaji kutoa cheti chake cha kuzaliwa hadharani.
Na Sarah Ferguson alizungumzia kwanini hakualikwa kwenye harusi ya kifalme Uingereza.
Kwahiyo ni namna gani ambavyo Winfrey ameweza kufanikiwa? Mambo 10 yanajumuisha ushawishi wake. 

MWAKA 1986 ALIDAI KUZALILISHWA KIJINSIA

  

Katika hatua yake ya kukiri ambapo baadae ikaja kuwa namna ambavyo anafanya kazi, Oprah aliwaambia watazamaji wake kuwa alibakwa alivyokuwa mtoto.
Si kwamba tu ilisababisha mwanzo wa kampeni isiyo rasmi kuhusu udhalilishaji, iliweka njia kwa msururu wa watu-maarufu wenye mtawaliwa, watu wa kawaida wenye mambo ya kueleza- kukaa kwenye kochi lake na kukiri.
Mwandishi wa vitabu Bonnie Greer, aliyeondoka kwao Chicago mwaka huo huo ambao Oprah alianza kupanda chati mjini humo, alisema: " Amefanya mawazo yaliyo ya wengi yakubalike kirahisi lakini anaielezea kama inamhusu moja kwa moja mwanamke wa Kimarekani mweusi.
"Imekuwepo siku nyingi katika utamaduni wa Kimarekani, lakini Oprah aliileta kwenye televisheni wakati wa mchana. Alianzisha utamaduni wa "mwathirika" kwa mantiki ya uzuri na ubaya.
"Aliingia wakati wa msukosuko wa uchumi katikam iaka ya mwisho ya 80 na mwanzo wa 90, jambo ambalo Wamarekani walitaka kuhakikishiwa: namna ya kuhimili na uzuri wetu.
"Oprah alizungumzia vitu kwa waliokuwa wakitazama vipindi vyake kwasababu alitaka kuonyesha 'uzuri' na 'uaminifu' yana malipo yake hapa duniani.


AFUNGUA SHULE SOUTH AFRIKA 2007

 

Shule ya uongozi ya Winfrey, karibu na Johannesburg, ilifunguliwa mwaka 2007 kwa gharama ya dola za kimarekani milioni 40.
Aliahidi kujenga shule hiyo baada ya kukutana na aliyekuwa rais wa Afrika kusini Nelson Mandela mwaka 2002.
Winfrey mwenyewe aliwahoji wasichana wengi wa Afrika kusini waliotoka kwenye familia maskini walioomba nafasi 150 za mwanzo katika shule hiyo.
Mwaka jana, aliyekuwa matroni wa chuo hicho alifutiwa mashtaka ya kudhalilisha mabinti chuoni hapo.
Winfrey alieleza namna alivyosikitishwa wakati hukumu ilipotolewa lakini alisema anajivunia kwa namna wasichana hao walivyopata ujasiri wa kutoa ushahidi.
Ufadhili wake unajulikana, na wakfu wake wa Oprah Winfrey umechangia mamilioni ya dola kwa miradi Marekani na nchi za nje, huku shirika lake la ihsani Oprah's Angel limechanga kiasi cha dola za kimarekani milioni 80.

KUAGA WATU KATIKA VIPINDI VYAKE VYA MWISHO 2011 
 

Moja ya vipindi vya mwisho vya Oprah Winfrey huko Chicago uligeuka kuwa usiku uliojaa machozi, shukrani na watu mashuhuri kama vile Tom Cruise, Will Smith na Madonna.
" Jambo kuhusu Oprah ambalo linapendeza ni kwamba ameweza kuunda alama inayojumuisha utata mkubwa.
" Ni rafiki yako halisi ambao marafiki zake ni Julia Roberts na Tom Cruise. Ni kiongozi wa dini anayefanya kazi kupita kiasi na hufanya kipindi kwa mwaka kuhusu vitu vyote vya gharama anavyopenda.
"Ni kiongozi wa dini asiyechagua kanisa lipi aende. Ni mwanamke anayeteta wazazi wa kike na desturi za kifamilia lakini binfasi hana watoto."
Utata huu unavutia wanawake, alisema." Wanashukuru kwamba wanaweza kumwangalia Oprah na kuona mtu kama rafiki yao wa karibu lakini pia huwapa nafasi katika ulimwengu huu mzuri."

OSAMA BIN LADEN 


 


Siku ambayo ndege zilizotekwa nyara ziligonga majengo ya World Trade Centre na makao ya wizara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ni vitendo vilivyombadilisha Osama bin Laden kutoka mtu mdogo asiyejulikana na kumfanya kuwa mojawapo watu wanaotambulikana sana duniani.

Bin Laden aliwahi kunukuliwa akisema: "Kile ambacho Marekani inakionja hivi leo ni kitu kidogo sana ikilinganishwa na kile ambacho tumekuwa tukikipata katika miongo kadhaa. Taifa letu limekabiliwa na hali hii ya kudhalilishwa na kudharaualiwa kwa zaidi ya miaka 80. Wanawe wanauwawa, damu yao inamwagwa, maeneo yake matakatifu yanahujumiwa na hayatawaliwi kwa mujibu wa amri zake Mwenyezi Mungu."
Osama bin Laden alizaliwa mwaka 1957 katika familia yenye utajiri mkubwa. Baba yake alianzisha kampuni kubwa ya ujenzi katika Saudi Arabia. Akiwa ni miongoni mwa ndugu 18 wa kiume, Osama aliwahi kufanya kazi katika biashara hiyo ya familia. Maisha yake yalianza kubadilika alipokuwa kijana pale Muungano wa Sovieti ulipoivamia Afghanistan.
Alipokwenda Aghanistan, Osama alikuwa kijana sana ambaye alitaka kujijengea umaarufu, katikati ya vita vitakatifu. Osama bin Laden alikaa kwa kipindi cha takriban miaka 10 nchini Afghanistan, na kuanzisha fungamano na wanaharakati wa siasa kali za kiislamu kote duniani.
Na baada ya majeshi yaliyovunjika moyo ya Sovieti kuondoka Afghanistan mnamo mwaka 1989. Osama bin Laden alirejea nyumbani Saudi Arabia. Mwaka mmoja baadaye alijitolea kumpa msaada wa kijeshi mfalme Fahad wakati Iraq ilipoivamia nchi jirani ya Kuwait. Lakini Osama alipatwa na mshtuko mkubwa pale Mfalme Fahad alipokataa toleo lake na badala yake kuigeukia Marekani.
Osama alinyaganywa uraia wa Saudi na akarejea Afghanistan ambayo wakati huo ikitawaliwa na Wataliban ambao alikubaliana nao kuhusu tafsiri ya uislamu.
Mnamo mwaka 1998 aliwahimiza waislamu wawauwe Wamarekani mkiwemo raia popote pale watakapowapata, kukafuatiwa mashambulio kadhaa ikiwa ni pamoja na dhidi ya balozi za Marekani katika Kenya na Tanzania na manowari ya USS Cole katika mwambao wa Yemen. Halafu shambulio la September 11, 2001.


Nyumba ambayo Osama alikutwa na kuuwawa. 

 


Osama bin Laden aliwasifu waliofanya shambulio hilo. Rais Bush akasema atasakwa apatikane akiwa hai au mfu.
Rais Bush alikunukuliwa kusema: "Sijui kama tutampata kesho au mwezi ujao au mwaka ujao. Lakini hapana shaka tutampata tu."
Ingawa Waislamu wengi walilaani vifo vya watu katika miji ya New York na Washington, Osama bin Laden alichukuliwa na wengi kuwa ni shujaa, aliyetetea haki za Wapalestina na kupinga nguvu za Marekani.
Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama bin Laden anaaminika kuacha watoto 17.

No comments:

Post a Comment