The hip hop legendary Jay-Z, hivi karibuni
ameziface camera na microphone za waandishi wa habari na kuelezea nini
kinachompa nguvu ya kumsapoti president Barack Obama kwa kumpigia kampeni kubwa
ili aendelee kuwa rais wa taifa hilo kubwa na lenye nguvu duniani.
Hivi karibuni Leotainment iliandika makala
maalum inayoelezea historia yenye matukio yanayoonyesha chanzo cha urafiki wa
Baraka Obama na Jay-Z, lakini hakuna hata msitari mmoja ambao ulionesha kuwa
Jay-Z anazifahamu siasa za Marekani ama aliwahi kujihusisha nazo kabla ya mwaka
2008, japo watu wengi sana hasa wa Marekani walianza kumtabiria Jay-Z kuwa ipo
siku anaweza kugombea nafasi katika serikali ya Marekani, background ya Jay-Z
hayajawahi kuwa na hata chembe ya Siasa. Swali likawa inakuwaje katika kipindi
cha kugombea urais wa Marekani kuanzia mwaka 2008 Jay-Z anaonekana yuko msitari
wa mbele kumpigania Obama, kualikwa mara kwa mara white house, lakini pia katika awamu hii ya pili
anaonekana yuko serious zaidi?
Jigga alipoulizwa kama anampango wa kujihusisha
na serikali ama siasa, alikiri kuwa hana nafasi yoyote na hana uwezo wa
kuchambua political game.
“silipendi hata hilo neno ‘Siasa’, alisema “It
implies something underhanded and I think we need less government,”Jay-Z
alifunguka alipokuwa katika club yake ya 40/40 kusherehekea ku-release rasmi
video game inayoitwa “NBA 2K13’ ambayo yeye mwenyewe aliipa title hilo kama
executive producer.
Jay-Z alijibu kiundani swali la wengi kuwa
ni kwa nini Obama na sio wengine waliopita, na kwa nini ameamua kumpa support
ambayo inaonekana ni ya hali na mali hadi kuanzisha fundraising program
iliyompa Obama zaidi ya $4 million kwa ajili ya kampieni? Alisema “namsupport
Obama kwa sababu inabidi niheshimu maono yaliyo ndani yake, inanibidi nimsapoti
mtu ambae ni rais wa kwanza mweusi ambae hajawi kutokea,” akaongezea kwenye
sababu hizi alisema “kwa kuwa na maono na ndoto kama hizi inanibidi nimsapoti.”
Katika kile ambacho wachambuzi wa mambo ya
siasa na wengine wanavyotoa sababu za yeye kuwa karibu sana na Obama tofauti
kabisa na hizi anazosema yeye, baba blue Ivy alikuwa na message kwa ajili yao
“napenda kuwa mkweli kwenu kuwa watu wengi sana wanaanzisha ajenda zao kwa
sababu zao tu, kwa hiyo wanajaribu kuzungumza vyovyote kwa kuwaza kuhusu
maslahi yao ya baadae,” alisema Jay-Z. Akaongezea hapohapo “watu hao wanawaza
kuhusu nafsi zao na sio kuhusu watu wote. Wanafanya lolote kuwaambia watu
lakini kitu kidogo ndicho kinafanyika kwa sababu they are going back and forth
with whatever they are doing,” na akamalizia kwa msisitizo kuwa “kwa hiyo mimi sipo katika siasa.”
Wiki iliyopita Barack Obama alihudhuria
tukio la kuchangia kampeni zake iliyoandaliwa na familia ya swaiba wake Jay-Z,
ambapo Jay-Z na mkewe Beyonce Knowles-Carter kwa pamoja walikusanya zaidi ya $4
million ambapo wageni mia moja walilipia tiketi za VIP ambapo kila tiketi
iligharimu $40,000, tukio liliofanyika kwenye club yao ya 40/40, ambapo the
R&B queen Beyonce alipanda jukwaani akiwa ndani ya gauni zuri jekundu na
kumtambulisha Barack Obama kwa wageni waalikwa.