Saturday, September 29, 2012

HIZI NDO SABABU ZINAZOMFANYA JAY-Z AMPE SUPPORT OBAMA KATIKA KAMPENI ZA KUWANIA URAIS.

 


The hip hop legendary Jay-Z, hivi karibuni ameziface camera na microphone za waandishi wa habari na kuelezea nini kinachompa nguvu ya kumsapoti president Barack Obama kwa kumpigia kampeni kubwa ili aendelee kuwa rais wa taifa hilo kubwa na lenye nguvu duniani.

Hivi karibuni Leotainment iliandika makala maalum inayoelezea historia yenye matukio yanayoonyesha chanzo cha urafiki wa Baraka Obama na Jay-Z, lakini hakuna hata msitari mmoja ambao ulionesha kuwa Jay-Z anazifahamu siasa za Marekani ama aliwahi kujihusisha nazo kabla ya mwaka 2008, japo watu wengi sana hasa wa Marekani walianza kumtabiria Jay-Z kuwa ipo siku anaweza kugombea nafasi katika serikali ya Marekani, background ya Jay-Z hayajawahi kuwa na hata chembe ya Siasa. Swali likawa inakuwaje katika kipindi cha kugombea urais wa Marekani kuanzia mwaka 2008 Jay-Z anaonekana yuko msitari wa mbele kumpigania Obama, kualikwa mara kwa mara white house,  lakini pia katika awamu hii ya pili anaonekana yuko serious zaidi?

Jigga alipoulizwa kama anampango wa kujihusisha na serikali ama siasa, alikiri kuwa hana nafasi yoyote na hana uwezo wa kuchambua political game.
 “silipendi hata hilo neno ‘Siasa’, alisema “It implies something underhanded and I think we need less government,”Jay-Z alifunguka alipokuwa katika club yake ya 40/40 kusherehekea ku-release rasmi video game inayoitwa “NBA 2K13’ ambayo yeye mwenyewe aliipa title hilo kama executive producer.
Jay-Z alijibu kiundani swali la wengi kuwa ni kwa nini Obama na sio wengine waliopita, na kwa nini ameamua kumpa support ambayo inaonekana ni ya hali na mali hadi kuanzisha fundraising program iliyompa Obama zaidi ya $4 million kwa ajili ya kampieni? Alisema “namsupport Obama kwa sababu inabidi niheshimu maono yaliyo ndani yake, inanibidi nimsapoti mtu ambae ni rais wa kwanza mweusi ambae hajawi kutokea,” akaongezea kwenye sababu hizi alisema “kwa kuwa na maono na ndoto kama hizi inanibidi nimsapoti.”
Katika kile ambacho wachambuzi wa mambo ya siasa na wengine wanavyotoa sababu za yeye kuwa karibu sana na Obama tofauti kabisa na hizi anazosema yeye, baba blue Ivy alikuwa na message kwa ajili yao “napenda kuwa mkweli kwenu kuwa watu wengi sana wanaanzisha ajenda zao kwa sababu zao tu, kwa hiyo wanajaribu kuzungumza vyovyote kwa kuwaza kuhusu maslahi yao ya baadae,” alisema Jay-Z. Akaongezea hapohapo “watu hao wanawaza kuhusu nafsi zao na sio kuhusu watu wote. Wanafanya lolote kuwaambia watu lakini kitu kidogo ndicho kinafanyika kwa sababu they are going back and forth with whatever they are doing,” na akamalizia kwa msisitizo kuwa “kwa hiyo mimi sipo katika siasa.”
Wiki iliyopita Barack Obama alihudhuria tukio la kuchangia kampeni zake iliyoandaliwa na familia ya swaiba wake Jay-Z, ambapo Jay-Z na mkewe Beyonce Knowles-Carter kwa pamoja walikusanya zaidi ya $4 million ambapo wageni mia moja walilipia tiketi za VIP ambapo kila tiketi iligharimu $40,000, tukio liliofanyika kwenye club yao ya 40/40, ambapo the R&B queen Beyonce alipanda jukwaani akiwa ndani ya gauni zuri jekundu na kumtambulisha Barack Obama kwa wageni waalikwa.

No comments:

Post a Comment