Sunday, June 24, 2012

VAZI LA HIJAB LAMZUIA MAMA HUYU KUSHIRIKI KIKAO CHA WAZAZI



Mwana mama Maroon Rafique miaka 40, anaeishi Wingereza alizuiliwa kuingia katika kikao cha wazazi katika  chuo cha Manchester alipoenda kwa ajiri ya mwanae.
Dada mmoja aliyekuwa mapokezi alimwamwambia Maroon kuwa hawezi kumruhusu mama huyo aingie katika kikao hicho akiwa kavaa hijab na huo ndio utaratibu.
Baada ya hapo alimbiwa ampigie mumewe simu aje kuhudhuria kikao hicho kuangalia maendeleo ya mtoto wao Awadh (18).
Maroon alisema "mwanagu yupo chuoni hapa huu mwaka wa pili na mimi nimeshawahi kuja chuoni hapa mara mbili bila matatizo yoyote, ila nashangaa leo yule dada mapokezi kaniambia siwezi kuingia bila kuvua hijab"
aliongeza na kusema " nilimwambia kuwa naweza nikakaa mbele au nyuma au popote ambapo sitamkera mtu, mi nimezaliwa nchi hii na ni Muingereza halisi kwanini ninachokivaa kimkere mtu"
Pia msemaji wa chuo hicho cha Manchester college alisema kuwa malalamiko ya mama huyo yanafanyiwa uchunguzi.


No comments:

Post a Comment