Sunday, June 24, 2012

DAWA ZA KUMBADILI BINADAMU KUWA ZOMBIE ZAGUNDULIKA

Dawa aina ya mind-bending narcotics zimegundulika kuwa zinamfanya mtumiaji kula binadamu mwenzake, dawa hizo ambazo gamba lanje zimeandikwa BATH SALTS zimeshasambaa katika nchi ya Marekani na Inasemekana Zinasafirishwa kutoka Wingereza.
                                

                                      FUATILIA MATUKIO YAFUATAYO

RONALD POPPO: mwenye miaka 65 uso wake ulitafunywa vibaya na RUDY EUGENE (31). Eugene alipigwa risasi na polisi hadi kufa  huko Miami baada ya kushindwa kujizuia na kuanza kuwaungurumia polisi mithili ya mnyama poli.





huyu ni RUDY EUGENE alitafuna uso wa RONALD POPPO kama unavyomuona hapo juu akiwa ameshikilwa na madaktari.




Alex Herriet (19) alifariki baada ya kutumia dawa hizo kwa kiasi kikubwa.



Pamela McCarthy umri miaka 35 alimtafuna mwanae wa kiume mwenye miaka mitatu, mwanamama huyu alishambuliwa na polisi na kufia hospitali baada ya kufeli uti wa mgongo.

Watumiaji wa madawa hayo walisema kuwa dawa hizo zinawafanya kujihisi joto sana na huwa wanapata nguvu za ajabu inyogharimu watu 6 hadi 7 kumzuia.
kumetanda hali ya hofu na tahadhari kwa sasa kuwa huwenda wakatokea Mazombi wa ukweli kama wale wa kwenye filamu mfano filamu ya DAWN OF THE DEAD.



 

No comments:

Post a Comment