Friday, June 15, 2012

SIMU INAYOFUKUZA MBU YAINGIA TANZANIA


TEKNOLOJIA ya kutumia simu kufukuza mbu nyakati za usiku imeingia nchini.Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Gerald Simbo aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana  kwamba simu yake ina uwezo wa kufukuza mbu usiku inapowekwa kwa kutumia mfumo wa 'Mosquito repellant'.

Simbo alisema simu yake inayojulikana  kwa jina la "Samsung Galaxy Pocket ina uwezo wa kufukuza mbu kama itawekwa kitandani wakati wa kulala.

Alisema simu hiyo aliinunua kwenye kampuni SamSung Tanzania. Meneja wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar alipoulizwa jana kuhusiana na kauli hiyo alikiri kuwa na aina hizo za simu na kwamba sasa zinasambazwa nchini na kuuzwa kwa gharama ya Sh200,000.

"Kwa ujumla simu hii ni ya kisasa  inayokidhi mahitaji ya mawasiliano kwa Watanzania na zaidi inakuja na ofa nyingine ikiwemo kadi ya simu na Airtel bundle, pia ina mfumo ambao endapo  itaibiwa mmiliki na uwezo wa kuifunga ,"alisema Kumar.

Naye mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Enock Kweka alisema anaitumia simu ya aina hiyo kufukuza mbu nyumbani kwake na  kuhifadhi nyaraka muhimu anazotumia katika masomo yake.Ilielezwa kwamba  ina mtandano wa kompyuta wa 250 MB kwa muda wa mwaka mmoja.
(kutoka:Mwananchi)

No comments:

Post a Comment