Mkurungezi
wa kampuni ya MSAMA PROMOTION ,Bwa.Alex Msama pichani mwenye fulana ya
mistari akiwaonesha waandishi wa habari Cds za video na Audio za Muziki
wa aina mbalimbali pamoja na Kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa
njia ya wizi kwenye kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma.
Jeshi
la Polisi mkoani Dodoma limeendesha Operesheni maalum ya kukamata
maharamia wa kazi za wasanii nchini na kufanikiwa kuwatia mbaroni
watuhumiwa 25 wakiwa na mashine za kurudufu CD na mali zingine zenye
thamani ya zaidi ya Milioni 67.
Kufanyika
kwa Opresheni hiyo kunafutia taarifa zilizotolewa na baadhi ya wasanii
nchini ikiwemo wa filamu, nyimbo za injili na Bongo fleva kulalamikia
kitendo cha baadhi ya wenye maduka ya CD mjini Dodoma kuuza kazi
zisizokuwa na hatimiliki zao.
No comments:
Post a Comment