
Kumekua na tabia ya kusafirishwa kwa mabinti kutoka nchi mbali mbali kuingia Wingereza,
Idadi hiyo ya mabinti hao sasa imefikia hadi 946 kwa mwaka na kati ya hao 234 ni watoto wadogo.
Mabinti hao wengi hudanganywa kuwa wanaenda kufanya kazi nzuri au kusoma na badala yake hulazimishwa kujiingiza katika biashara za uchangudoa ama kufanywa kama watumwa na kufanyishwa kazi viwandani na mashambani.
Wengi wa mabinti hao huchukuliwa kutoka Romania,Vietnam, China na Nigeria.
No comments:
Post a Comment